Ukubwa wa stori hii ambayo jana aliizungumzia
Martin Kadinda kama Meneja wa Wema Sepetu
imefanya millardayo.com kutaka kuujua undani
zaidi kutoka kwa Wema mwenyewe.
Kwenye exclusive Interview,Wema
amesema>>’Taarifa hii imenishtua sana maana
asubuhi ya jana nimekuta kwenye gazeti
wameandika nikashangaa yaani hapa nimekaa
kwa sababu muda mwingi siendeshi mimi akaunti
yangu ya twitter,anaiendesha mtu wangu wa blog
Bestizo maana nilikua nataka kutoa tamko’
‘Nilishasema ukurasa huu tulishaufunga na
nilishasema haiwezi kujirudia tena,nashangaa
watu wanarudi na maneno yale yale maana
nimekaa kimya kwa kila kitu ili kuepuka haya
maneno’
‘Hakuna kitu ambacho namdai Diamond,hakuna
siku hata moja nimefikiria kwenda kumshtaki
Diamond labda kama kungekua kuna kitu
chochote,yaani labda kungekua na ukweli wa kitu
chochote siwezi kupoteza muda wangu kwenda
polisi,sijawahi kufanya kitu cha namna hii hizi
taarifa zimenishtua sana’
‘Sijawahi kujiunga Vikoba maana sivijui,nilikua
nimekaa na mtu akanambia labda Wema hujui
hawa watu wa vikoba wanajaribu kujitangaza kwa
njia hii na kutengeneza hii kitu kwamba vikoba
wanaweza kukopa hadi Milioni kumi kwanza mimi
siwezi kukopa Milioni 10′.