Friday, January 9, 2015

DUDE: FILAMU KWA BUKU, ‘NO’, NASEMA NOOO!

Staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude.
Stori: Shani Ramadhani
Staa wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameiomba serikali iwasaidie kutokana na mpango uliowekwa wa kuuzwa filamu zao kwa shilingi elfu moja, jambo ambalo anaona litawafanya wasanii wazidi kuwa masikini.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Dude alionesha kutokukubaliana na hatua hiyo na kueleza kuwa, endapo serikali italifumbia macho suala hilo, soko la filamu litakufa.
“Yaani nasema noooo, kiukweli filamu kuuzwa bei ya shilingi elfu moja wasanii tutakuwa hatuioni faida, ni bora hata ingekuwa shilingi elfu mbili na kukazana kufanya msako wa wale wezi wa kazi za wasanii, kidogo ingekuwa afadhali,” alisema Dude.
Mpaka sasa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imetoa tamko kuwa inashughulikia malalamiko hayo ili kuona kinachoweza kufanyika katika kuinusuru tasnia hiyo.