Friday, January 9, 2015

ROSE MUHANDO AWEWESEKA

Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando.
MWIMBAJI nyota wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando ambaye hivi karibuni alikanwa na aliyewahi kuwa meneja wake wa muda mrefu, Alex Msama, anadaiwa kuweweseka asijue la kufanya kufuatia hatua hiyo.
Akizungumza kutoka Dodoma yalipo makazi ya mwimbaji huyo, mmoja wa watu wake wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema hatua ya Msama kutangaza kutofanya naye kazi, limekuwa pigo kwake kwani ndiye aliyekuwa kiongozi na mwokozi wake wa mambo mengi ya kikazi na binafsi.
Meneja wa Rose Mhando, Alex Msama.
“Anaweweseka kwa kweli na hajui la kufanya, Msama ndiye alikuwa msaada wake mkubwa kwa kila kitu kuhusiana na muziki japo kwa sasa amekuwa hataki hata kumsikia Rose,” alisema mtu huyo.
Rose alipigiwa kutaka kusikia kutoka kwake, lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi ulionyeshwa kupokelewa bila majibu. Msama alipoulizwa kuhusu kilio cha msanii huyo alisema yeye ameshatoa msimamo wake na unaeleweka.