Mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally ‘Mama Sasha’ amewafungukia watu ambao wanamponda yeye kutinga na ‘pampers’ ukumbini na kusema kuwa hiyo ni moja ya maamuzi yake binafsi.
Mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally ‘Mama Sasha’ akipozi.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Faiza aliyetinga vazi hilo katika siku yake ya kuzaliwa hivi karibuni, alisema kuvaa vile hafikiri kama kuna ubaya kwa mtu yeyote kwa kuwa kila mmoja ana maamuzi yake na hakumdhuru mtu.
“Mimi na maamuzi ya kuvaa chochote ambacho najisikia na kama hakina shida na mtu nakivaa na kuvaa vile ni moja tu ya kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa na nilitaka kuwa tofauti,” alisema Faiza kuwajibu wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakimponda mtandaoni juu ya tukio hilo.