Friday, January 23, 2015
HAKIELIMU WAPONDA MPANGO WA MATOKEO MAKUBWA SASA (BRN) KATIKA ELIMU
Shirika la haki Elimu nchini Tanzania limetoa tathmini ya mpango wa matokeo makubwa sasa BRN katika sekta ya elimu kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita inayoonesha kwamba hali ya utekelezaji wa mpango huo si ya kuridhisha.
Kaimu mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Godfrey Boniventura amesema kuwa pamoja na serikali kutambua kuwa sekta ya elimu hapa nchini ina changamoto nyingi na kuonesha nia ya kukabiliana na changamoto hizo kwa kubuni mipango mbalimbali kama ya BRN lakini bado juhudi kubwa zinahitajika.
Amesema serikali isitumie kigezo cha kuongezeka kwa ufaulu unaoonekana kupanda ghafla kwa kuwa changamoto zilizopo katika sekta ya elimu ni nyingi na bado hazijatatuliwa zikiwemo za wanafunzi kukaa chini kwa kukosa madawati, vifaa vya kufundishia ni vichache huku maabara zikitajwa kuwa ni chache na hazina vifaa.
Kwa upande wao wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wamekuwa na mawazo tofauti ambayo ni chachu kwa wizara ya elimu endapo watayafanyia kazi maoni hayo, tatizo hilo litapungua
WAGOMBEA UDIWANI WATAKIWA KUPIMA VIRUSI VYA UKIMWI KABLA YA KUCHUA FOMU ZA KUGOMBEA