Happiness ameimbia Paparazi kuwa ingawa hakushinda taji la Miss World, umoja uliooneshwa ni ushindi tosha.
“Nimekuja kutoa shukrani zangu kwa watanzania kwa kupiga kura na kunipa support. Mimi sidhani kwamba ni bahati mbaya kushindwa na haya matokeo sio kwamba nimefurahi ila nimetaka kuwa kama daraja ili wengine wapate urahisi. Najisikia ni kama tumetengeneza njia. Nimefanya kazi mwenyewe nimepata watu ambao wametoa muda wao kunisaidia na tumefanya kitu kikubwa sana kwahiyo huo ni kama msingi ambao utasaidia wengine,” ameongeza.
Katika hatua nyingine Happiness amesikitishwa kwa kufungiwa shindano la Miss Tanzania licha ya kuwa na kasoro kadhaa.
“Ni kitu cha kusikitisha kwa sababu kuna wasichana wengine wengi ambao wanataka kuwa Miss Tanzania na wanataka kuleta mabadiliko katika hii nchi kupitia nafasi hiyo. Lakini pia nadhani kuna mapungufu kadhaa katika shindano lenyewe, nafikiria ni kitu cha kuusaidia uongozi na watu wote ambao wapo related na hilo shindano. Kurudi nyuma na kuangalia nyuma wapi wanaweza kujirekebisha.”