Tuesday, January 6, 2015

SAMAHANI KWA PICHA HII: MWANAUME ACHOMWA NA MAJI YA MOTO SEHEMU ZA SIRI NA MKEWE KISA WIVU WA MAPENZI


Mwanamke mmoja ambaye jina lake ni Nomsa Dube mwenye umri wa miaka 28 amemchoma mumewe sehemu za siri kwa maji ya moto baada ya kuhisi akiwa namsaliti na mwanamke mwingine.

Mwanaume huyu ambaye jina lake ni Fezile Dube’s (35) ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya uvimbe sehemu zake za siri na walipomfuata daktari aliwa waambia kwamba mwanaume huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa hata wa mkanda wa Jeshi ambapo daktari alisisitiza mwaume huyo kurudi baada ya miezi mitatu ili kuja kufanya vipimo vya ugonjwa wa Ukimwi baada ya miezi mitatu.

Baada ya kurudi nyumba mwanaume huyo alikiri kuwa na wasichana ambao alikuwa akilala nao nje ya ndoa yake, na mkewe baada ya kuambiwa hivyo alianza kumlaumu na kumuliza kwanin hakutumia kinga.

Licha ya mwanaume kuwa na michepuko nje ya ndoa yake lakini ilikuwa tofauti kwa mkewe ambaye alikuwa muaminifu kwa mumewe ndipo alipokasirika na kumchoma na maji ya moto kwa mujibu wake anasema mumewe anabahati sana kutokana na kwamba hakumwambukiza laiti kama angelikuwa kamuambukiza basi angefanya kitendo cha kikatili zaidi ya kumchoma na maji ya moto mumewe.