Nay wa Mitego amempongeza Nikki Mbishi kwa uamuzi wake wake kuachana na muziki.
Hata hivyo Nay amesema Nikki amechelewa mno kufanya hivyo.
“Mtu unaweza kuangalia hiki hakinifai bora niende upande mwingine labda unaweza ukagharamia kitu ukakuta sio sehemu ambayo umepangiwa, ukaenda ukajaribu kitu kingine ukakuta maisha ni rahisi na yanaenda, Nay amekiambia kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio.
“Sijui kwanini alikuwa anachelewa, nimefurahi kuona maamuzi mazuri kijana mwenzangu amejitambua na kuamua kuangalia vitu vingine. Kama bado hajapata cha kufanya aje mimi nimshauri afanye nini.”