Mgogoro unaoendelea ndani ya klabu ya Barcelona kwa sasa umezua tetesi nyingine kuhusiana na baadhi ya wachezaji ambao wanaweza kuihama klabu hiyo baada ya hali kuonekana sio nzuri kutokana na matokeo ya timu hiyo kutokuwa mazuri .
Mchezaji nyota wa timu hiyo Lionel Messi ambaye majuzi aliwekwa benchi wakati wa mchezo wa Barcelona dhidi ya Real Sociedad amehusishwa moja kwa moja na kinachoendelea ndani ya Barcelona kwa sasa .
Inadaiwa kuwa uhusiano wa Messi na kocha wake Luis Enrique si mzuri kiasi cha kufikia hatua ya nyota huyo kukosa raha ndani ya klabu hiyo .
Hali ya Messi kutoelewana na kocha wake imezua tetesi za nyota huyo kufikira kuihama Barcelona japo hakujawa na taarifa rasmi toka kwake au wawakilishi wake kuthibitisha habari hizi .
Watu wanaofuatilia mitandao ya kijamii walua maswali mengi baada ya Messi kuufuata ukurasa rasmi wa klabu ya Chelsea kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kitendo ambacho kimehusishwa na nyota huyo kuwa na mawazo ya kuhamia huko .
Kama hiyo haitoshi mpenzi wa Messi maeonekana akiufuata ukurasa wa mpenzi wa nyota wa Chelsea Cesc Fabregas na wadadisi wa mambo wameunganisha matukio haya na kuzua tetesi ya Messi kuwa na mpango wa kuhamia jijini London kwenye klabu ya Chelsea.