Monday, January 12, 2015

JOKATE:SIJAWAHI ‘BANJUKA’ NA MILLARD AYO!

MTOTO mzuri mwenye taito kubwa katika anga la mitindo Bongo, Jokate Mwegelo ameucho molea vilivyo uvumi uliozagaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji Millard Ayo wa Clouds FM.
Mtoto mzuri mwenye taito kubwa katika anga la mitindo Bongo, Jokate Mwegelo akipozi kimahaba na mtangazaji Millard Ayo wa Clouds FM.
Uvumi huo ulianzia mitandaoni ambapo mwanahabari wetu alipomtafuta Jokate juzikati, aliweka plain ukaribu wake na Millard ambaye ni mtangazaji mwenye mvuto mkubwa kwa jamii.
“Millard ni mshkaji, namkubali kutokana na uchapakazi wake, anajua kujituma na ni mpambanaji lakini nje ya hapo hakuna cha zaidi,” alisema Jokate.