Monday, January 12, 2015

SUZY AKATAA KUITWA BONGO MOVIE

MSANII anayezidi kuja kwa kasi Bongo Movies, Happy Nyatawe ‘Suzy’ ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa kutokana na migogoro mbalimbali iliyokuwepo ndani ya Kundi la Bongo Movie, hata akipita njiani akiitwa kwa kutumia jina hilo hatogeuka.
Msanii anayezidi kuja kwa kasi Bongo Movies, Happy Nyatawe ‘Suzy’ akipozi.
Suzy alisema kutokana na ‘majanga’ kuwa mengi kundini, imefika hatua anaona hata aibu kujitambulisha kuwa yeye ni msanii kutoka Kundi la Bongo Movies.
“Kweli kabisa, mimi nikiitwa tu msanii wa Bongo Movie nikiwa napita njiani, sigeuki ng’o wataita mpaka wachoke kabisa, hali ni mbaya Bongo Movie tubadilike,” alisema Suzy.