Monday, January 26, 2015

LUIZA MBUTU AMTAJA BANZA KUWA NDIYE ALIYEMFUNDISHA AISHA MADINDA KUVUTA UNGA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE!

Msanii wa bendi ya Twanga Pepeta,Luiza Mbutu amesema kilichomfanya Aisha kutumia madawa ya kulevya ni uvutaji sigara uliompelekea kuvuta bangialiyofundishwa na Banza. Banza alikuwa anamchanganyia bangi na unga hadi ikafikia hatua ya kuwa addicted na na unga. Kabla ya Aisha kuaga dunia alikuwa ameachana na madawa ya kulevya,na kwenda Dubai kwa kudanganywa ni maswala ya bendi. Kumbe ni kwenda kuwa mfanyakazi wa ndani. Ndipo baada ya kukataa wakamnyang'anya pasport yake,ndipo akaenda kushtaki ktk ubalozi wa huko na kurudi Tanzania,akakutana na mashoga zake ambao alikuwa anatumia nao akawa anaendelea kutumia huku akiwa anatumia dawa za kuacha kutumia unga hadi kufikwa na mauti.
 Source: Radio Tumaini