Monday, January 5, 2015

MANAIKI: NATAKA KUPELEKA POSA KWA WOLPER

MSANII wa sinema za Kibongo, Manaiki Sanga ametangaza nia ya kutaka kwenda kupeleka posa kwa staa wa sinema, Jacqueline Wolper, kwa madai kuwa anampenda sana.Akizungumza  na mwandishi wetu, Manaiki alisema hapa Bongo wanaume wengi hawajui wanawake wazuri lakini kwa upande wake ameona uzuri wa Wolper ni pambo la moyo wake, atapeleka barua nyumbani kwao.
Msanii wa sinema za Kibongo, Manaiki Sanga akipozi na staa mwenzie, Jacqueline Wolper.
“Ni maoni yangu, mwaka huu mwanzoni napeleka posa kwa wazazi wa Wolper naamini ndiye mwanamke ambaye anafaa kuwa mke wangu labda tu tatizo kubwa liwe kwake lakini siwezi kubadilisha nia yangu,” alisema Manaiki ambaye anatarajia kutoa filamu yake inayoitwa AMKA aliyowashirikisha mastaa kibao kama Kajala, Majuto, Hemed, Mlela na wengine kibao.