Monday, January 5, 2015

KAJALA: UBONGE UNANIPA STRESS

STAA wa filamu mwenye mvuto wa aina yake Bongo, Kajala Masanja amesema kuwa hakuna kitu kinachompa ‘stress’ kama unene hivyo ameamua kuanza mazoezi.
Staa wa filamu mwenye mvuto wa aina yake Bongo, Kajala Masanja.
Akizungumza na mwandishi wetu, Kajala alisema hakuna kitu ambacho kinampa ‘stress’ kama unene hivyo kuanzia sasa ameamua kuacha usingizi wake kila asubuhi ili kufanya mazoezi ya kupunguza mwili.
“Unene ni stress jamani, sihitaji kabisa ni bora niache usingizi nifanye mazoezi na sasa hivi nimeshazoea na matunda ya kufanya mazoezi nayaona ni mazuri, sitaki kabisa unene,” alisema Kajala.