Monday, January 5, 2015

LULU AMZAWADIA MAMA’KE NYUMBA

Imekaa poa sana! Taarifa tamu ikufikie kwamba sexy lady wa Bongo Movies, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ amemfanyia mama yake, Lucresia Karugila kufuru ya kufa mtu kisha kumzawadia ile nyumba yake anayoimalizia iliyopo Kimara jijini Dar.
Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Tukio hilo la kupongezwa lilichukua nafasi usiku wa Januari Mosi, mwaka huu ndani ya Hoteli ya Great Wall iliyopo Masaki, Dar, ambapo Lulu alimfanyia mama yake pati ya bethidei akiwa anatimiza umri wa miaka 45.
Katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kadhaa Bongo na kufunika kwa mnuso wa nguvu na vinywaji vya kila aina, Lulu alitumia shughuli hiyo kuelezea ni kwa jinsi gani mama yake amekuwa msaada wake mkubwa na kuvumilia aibu zake katika jamii.
Shushushu wetu aliyekuwa ndani ya shughuli hiyo alimshuhudia Lulu akitoa risala ndefu kwa mama yake hivyo akasema mbali na kuandaa sherehe hiyo hana kingine cha kumpa mama yake zaidi ya kuongeza upendo na kumzawadia mjengo huo ambao kwa sasa upo vizuri.
‘Lulu’ akiwa na bi mkubwa wake, Lucresia Karugila.
Baada ya hapo, Lulu aliwashukuru wote waliomtakia heri mama yake na kuhudhuria sherehe hiyo.
“Napenda kuwashukuru wote mliomtakia heri ya kuzaliwa mama angu.
“Nawashukuru wote mlioweza kutumia muda wenu mkakubali mwaliko na mkafika katika sherehe maalum iliyoandaliwa kwa ajili yake.
“Najua nina ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wengi japo ni wachache tu walioweza kuwepo.
“Mwisho kabisa namshukuru mama Lulu kwa jina lingine dada wa Rwechungura,” alisema Lulu ambaye anaishi kwenye mjengo wa kifahari wa kupangisha uliopo Mbezi-Beach jijini Dar.