Monday, January 5, 2015

MUME, MCHEPUKO WAGOMBEA MTOTO

Makubwa! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mke wa mtu aliyekuwa akiishi ukweni na mumewe wa ndoa, Bahati Ramadhani, amenusurika kuuawa na ndugu wa mumewe wakiwemo mawifi na wakwe zake baada ya kudaiwa kumgonganisha mumewe na mchepuko wake na kujikuta wakigombea mtoto.
Mwanamke, Bahati Ramadhani anayeidaiwa kumgonganisha mumewe na mchepuko.
Tukio hilo la kushangaza lililojaza kadamnasi lilijiri nyumbani kwa wakwe hao, Mtaa wa Mawenzi jirani na Soko la Matunda la Mawenzi la mjini hapa wiki iliyopita ambapo Bahati alikuwa akiishi na mumewe, ldd Yusuf.
Ilielezwa kwamba wanandoa hao walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume (jina kapuni) ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 2.
Polisi akimbana kwa maswali mwanamke huyo kuhusu utata uliotokea.
Siku ya tukio, mama mkwe wa Bahati, Faidha Cosmas alishtukia dili baada ya kuona sms ya mwanaume ‘aliyeseviwa’ kwa jina la Saddy kwenye simu ya Bahati ikimweleza kwamba alikuwa amemtumia fedha za matumizi ya mtoto wao huyo.
Baada ya mama mkwe kuona ishu hiyo alimwambia mwanaye Idd ambapo kwa pamoja walimpigia Saddy aliyekiri kuwa anachojua mtoto huyo ni wake na amekuwa akituma fedha za matumizi.
Mama mkwe alisema kwamba walimwita Bahati na kumuuliza kama anamfahamu Saddy ambapo alikiri kuchepuka.
Mwanamke, Bahati Ramadhani akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Baada ya mzozo wa hapa na pale, mawifi wa Bahati waliingilia kati na kuibua bonge la mtiti wakimpa wifi yao kipigo hadi mwandishi wetu alipotonywa na kufika eneo la tukio.
Alipofika mahali hapo na kuona hali ya hatari ndipo akaita polisi wa doria ambao walifika na kutuliza ghasia.
Familia hiyo ilishuhudiwa ikiwa kwenye kikao ambapo uamuzi wa awali ulikuwa ni ldd kumuacha mara moja Bahati.
Wananchi wakishuhudia mkasa huo kwenye eneo la tukio.
Hata hivyo, katika uamuzi huo wa awali, Bahati alikubali kuondoka lakini kwa masharti ya kuondoka na mwanaye jambo ambalo liliikera familia hiyo na kumvamia wakitishia kumtoa roho.
Kabla ya mambo kuwa mabaya, polisi wakiongozwa na Afande Mwajabu waliingilia kati na kumuokoa Bahati.
Afande Mwajabu aliwahoji wahusika na baada ya maelezo, ldd alitoa uthibitisho wa kadi ya kliniki ambayo ilionesha yeye ndiye baba halali wa mtoto huyo.
Katikati ni mtoto anayegombewa katika utata uliojitokeza.
Mwandishi wetu pamoja na Afande Mwajabu walimpigia simu Saddy ambaye kwa sasa yuko masomoni mkoani lringa na kuweka ‘loud speaker’ ambapo alipoulizwa alisema:
“Mtoto ni wangu. Kwa sasa ana umri wa miaka 2 na kadi ya kliniki ninayo.”
Saddy alipoulizwa na mwandishi wetu kwa kipindi chote cha miaka miwili, mtoto wake alikuwa akiishi wapi alisema:
Mwanamke aliyegonganisha wanaume akichepuka akichukuliwa na mapolisi kutoka eneo la tukio.
“Nilikuwa bize na masomo lakini najua mwanangu yuko na mama yake.”
Kwa upande wake, Idd ambaye ndiye anayeishi na Bahati (huku akitokwa machozi) alisema hakutarajia kama mkewe angemsaliti kiasi hicho.
Bahati alipohojiwa, alisema kuwa siku aliyopata ujauzito alitembea na Saddy pamoja na mumewe ldd hivyo hata yeye anashindwa kujua baba halali wa mtoto wake.
Sakata hilo lilifikishwa polisi ambapo bado linatafutiwa suluhu.