Diamond Platnumz ni msanii ambaye huwa hafanyi makosa pale anapopata mwanya wa kukutana na fursa zinazoweza kumpa hatua hatika muziki wake.
Diamond na Peter Okoye wa P-Square
Mwimbaji huyo wa ‘Nitampata Wapi’ alipokuwa Nigeria hivi karibuni alipata nafasi ya kukutana na wasanii wakubwa wa Afrika wakiwemo P-Square, Fally Ipupa, Flavour na wengine. Na kwa mujibu wa kanuni yake huwa hafanyi makosa anapopata nafasi kama hizo.
“Mimi kanuni yangu kama ilivyo, nikikutana na 18 huwa siachi yaani naachia bonge la shuti mpaka nishinde kwahiyo vitu vyote vimekaa vizuri, lakini sio vizuri kuongea sana kwasababu vitu vingine bado viko chini ya kapeti…so watu wategemee vitu vizuri najitahidi sana kwenda resi na speed zote pale napofikia mimi niweze kufanya kitu kiwe kizuri.”Ameiambia E-Newz ya EATV.