Thursday, January 8, 2015

MTUHUMIWA WA MAUAJI ATOROKA CHINI YA ULINZI HOSPITALINI..ASKALI MAGEREZA ALIYEKUWA ANAMLINDA KUFUNGULIWA MASHTAKA...SOMA ZAIDI




MSHITAKIWA wa kwanza, Salim Marwa katika kesi ya mauaji ya raia wa Ghana, Joseph Opong ametoroka chini ya uangalizi akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam. 

Mkuu wa Magereza mkoa wa Dar es Salaam, Joel Bukuku alikiri kutokea kwa tukio hilo Jumatatu usiku majira ya saa 6:00 huku akiwa na askari magereza wawili. Alisema mshtakiwa huyo alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

Lakini hakufafanua zaidi kuhusu upasuaji wa nini wala alilazwa kwa muda gani. Kuhusu alikotorokea mshitakiwa huyo alisema bado magereza haijafahamu alikoelekea na kwamba tayari wametoa taarifa katika Jeshi la Polisi ili kuweza kusaidia kupatikana kwake.
Aidha, alisema tayari wamesambaza askari kwa ajili ya kumtafuta ili kukamatwa na hatua nyingine kufuatia.

Kuhusu askari waliokuwa wakimlinda alisema hajui kama kutoroka kwa mshtakiwa huyo chini ya uangalizi wao ni uzembe, lakini kwa kuwa wanazo sheria zao za Magereza watawafungulia mashtaka, kuwachunguza na kisha hatua nyingine zitafuata.

“Mimi kwa sasa niko nje ya ofisi, siwezi kuzungumzia zaidi kama mshtakiwa alikuwa akisumbuliwa na nini na alilazwa hospitalini hapo kwa muda gani…na hivyo sina details (taarifa) zaidi,” alisema Bukuku.

Marwa anashitakiwa kwa mauaji ya kikatili ya raia wa Ghana, Joseph Opong huko Bagamoyo mwaka 2010 ambapo alikuwa rumande kipindi hicho katika jela ya Keko hapa Dar es Salaam kabla ya kufikishwa hospitalini. Mbali ya Marwa ambaye inadaiwa alisomea urubani, mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo ni Peter Charles Mayalla.

Inadaiwa kuwa Septemba 10, 2010, washitakiwa hao walimuua kwa makusudi Opong, kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili, baada ya kumlewesha kwa dawa za kulevya na kisha kwenda kumzika katika msitu wa Kaole.

Akizungumzia tukio hilo, Mganga mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Amani Malima alisema hana taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kufuatilia zaidi ili kujua ukweli wake.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Temeke, Kihenya Kihenya alisema jeshi hilo halina taarifa za tukio hilo, akidai kuwa hawajapata taarifa