Msanii maarufu wa bendi na ambaye pia muigizaji wa Bongo Movie, Patcho Mwamba amemsamehe aliyemzushia kuwa amepigwa baada ya kufumaniwa na mke wa mtu kwenye hotel ya Sinza.
Kupitia mtandaoni aliyedaiwa kumzushia jamaa alitwaye Seth ameonekana amepiga picha na Patcho na kuandika kuwa ameomba msamaha na kwamba alikurupuka kuandika bila kufanyia uchunguzi habari hiyo.
Kupitia mtandaoni aliyedaiwa kumzushia jamaa alitwaye Seth ameonekana amepiga picha na Patcho na kuandika kuwa ameomba msamaha na kwamba alikurupuka kuandika bila kufanyia uchunguzi habari hiyo.
Kupitia Instagram bikira_wa_kisukuma aliandika hivi
LE TAMKOZZ:
Kwa wale ambao wamesikiliza YOU HEARD ya Sudi Brown mchana na AMPLIFAYA usiku huu watakuwa walisikia habari hii kutuhusu Mimi na Patcho Mwamba kuhusu habari zilizosambaa siku ya Krismasi na kufowadiwa sana kwenye Whatsapp na Meseji za Kawaida kwamba Patcho amefumaniwa...Watanzania wengi ikiwemo mimi hukurupuka na tetesi za vitu bila kubalance story na kuposti na sometimes vitu hivyo huwa ni Uzushi na Uongo...Mimi kama Seth,kama mmoja ya watu walioingizwa mkenge na stori hii na nikaishare kwa dakika 5 tu kwenye Page yangu na ikaleta usumbufu mkubwa kwa Patcho,familia yake,mashabiki na marafiki zake I feel Obliged kuomba msamaha IN PUBLIC...Sijali kama wengine walioshare wataguswa kusema SAMAHANI ila mimi nimeamua kutumia Page Hiihii kuwaambia WATANZANIA waliosikia Stori kuhusu Patcho kwamba NI UONGO na Patcho ana Allergy ya Pombe na nimelithibitisha hilo,na kwa sasa anaendelea vizuri kabisa baada ya kupata dawa kama mnavyomuona pichani..
USHAURI:Kabla hatujadandia vitu na kuvishare au stori ni vizuri kupata uhakika kwanza kabla ya kuviposti..
Im glad tumekutana na Patcho na kuongea na kuyamaliza,Mwaka uishe kwa Amani na Tusambaze Upendo..PEACE AND LOVE TO Y'ALL
You can share this to all friends waujue ukweli...Cheers!