Friday, January 9, 2015

PENZI KINYUME NA MAUMBILE LAMTESA LUNGI

Msanii wa filamu za Kibongo, Lungi Maulanga.
Stori:Laurent Samatta
MSANII wa filamu za Kibongo, Lungi Maulanga, amesema kuwa mpenzi wake amekuwa akimsaliti kila kukicha huku akihisi kuwa, huenda wanawake anaowafuata huko nje wanampa mapenzi kinyume na maumbile.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Lungi alisema kuwa siku chache zilizopita alilia sana kutokana na usaliti aliofanyiwa na mpenzi wake aliyemhifadhi kwa jina, akasema aliamua kumsamehe kwa kuwa anampenda.
“Naumia sana na nalia kila ninapokumbuka namna mpenzi wangu anavyonisaliti, sielewi ni kwa nini wakati mimi ni mrembo na nina umbo zuri ambalo kila mwanaume akiniona lazima anitamani.
“Nashangaa mwenzangu anavyochepuka, sijui huko nje anawafuata wale wanaotoa ‘mtandao’?” alihoji Lungi na kuongeza: “Mimi siwezi kumsaliti hata iweje, najua huko nje magonjwa ni mengi.”