Kama mnavyojua, siku ya jana hapa jijini Dar es salaam kulikuwa na taharuki kubwa ikiwahusisha baadhi ya vijana wanaojikusanya kwenye vikundi na kujiita Panya road ambao huzunguka mitaani kufaya vurugu na kupora watu na hivyo kusababisha hofu kubwa kwa wakazi wa jijini hapa.
Hivi ni vituko vya waigizaji Mzee Majuto na Nisha kwa nyakati tofauti, Mzee Majuto akiwa nje ya jiji la Dar, akionekana “anagonga” mchemsho wa samaki huku anaongea na simu, JB alimuwekea maneno haya kwenye picha hiyo;
Hallow poleni sana Dar na panya road.Huku ni raha tu.poleni sanaaa.hahaha
Hii iliwavunja mbavu watu kibao huko mtandaoni nakupokea 'Likes' za kutosha.
Wakati wigizaji Nisha akiwa amebebelea silaha mbalimbali, kama panga, shoka na kuzitupia video na picha mabilmbali mtandaoni na kuandika kuwa yupo kwenye msako kuwatafuta hao panya road.
Mwishoni akatupia picha hiyo na kuandika “Wakijitokeza tena mnibeep 000000”
Ila wengi walisema kama Nisha anaogopa , na kama wangetokea hapo angetoka nduki....wewe umemuonaje hapo, angewaweza kweli?.