Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford.
STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford amesema kuwa mara kadhaa anapokuwa lokesheni akishuti filamu mume wake, Dickson Matoke huwa anamfuata na kulala naye hadi asubuhi huku akiamini kufanya hivyo kunachangia kutochepuka.
Akizungumza na paparazi, Shamsa alisema kuwa kitendo cha mumewe kumfuata haina maana kwamba wanavunja sheria zao bali hilo analifanya kwa kuwa yeye ni mke wa mtu na huwa anapewa chumba chake maalum.
“Mara nyingi ninapokuwa lokesheni kama si mbali na nyumbani basi naenda kumuona mume wangu na mtoto lakini kama ni mbali kidogo mume wangu huwa anakuja na kulala na mimi chumbani kwangu, asubuhi anaondoka naendelea na kazi yangu,” alisema Shamsa.