Friday, January 16, 2015

STARA THOMAS AMKATIKIA MAUNO MZEE CHILLO

MWANAMUZIKI Stara Thomas juzikati aliwaacha watu hoi kwa kicheko pale alipoamua kumkatikia mauno Mzee Chillo walipokuwa wakicheza muziki.
Mwanamuziki Stara Thomas akikata mauno mbele ya Mzee Chillo.
Tukio hilo lililonogesha shughuli lilijiri kwenye uzinduzi wa kitabu cha marehemu Steven Kanumba kilichopewa jina la The Great Follen Tree uliofanyika ndani ya Hoteli ya Landmark, Ubungo jijini Dar.
Ilikuwa hivi; wakati wa kucheza muziki, kila mmoja alimvutia karibu yule aliyemvutia ambapo Stara aliamua kujongea kwa Mzee Chillo kisha kuanza kucheza taratibu lakini kadiri mambo yalivyonoga, mwanamama huyo alionesha umahiri wake wa kukata mauno na kumuacha mwezake akiangua kicheko.