Friday, January 16, 2015

MUME WANGU SIKUMUIBA KWA RAFIKI YANGU- VANITHA

Wiki hii kupitia safu hii tunaye staa wa filamu za Kibongo Vanitha Omary. Amebanwa maswali mengi na mwandishi wetu Hamida Hassan lakini kutokana na jina la kolamu hii, tunakuletea maswali 10 ‘hot’ aliyoulizwa na yeye kutoa ushirikiano katika kuyajibu licha ya kwamba aliachwa kijasho chembamba kikimtoka.
Staa wa filamu za Kibongo Vanitha Omary.
Ijumaa: Kuna hizi tetesi kwamba huyu mume wako wa sasa alikuwa ni mpenzi wa rafiki yako Joan Matovolwa lakini wewe ukampora na mkaishia kuoana, hili unalizungumziaje? Vanitha: (Kicheko) Ukweli ni kwamba mimi na Joan ni marafiki wakubwa na hilo unaloongea halina ukweli wowote. Maneno hayo yaliibuka baada ya kuwepo taarifa kuwa nataka kuolewa.
Ijumaa: Wewe ni msanii lakini ni mke wa mtu, siku ukiwa hujaenda kwenye shughuli zako za kisanii uwapo nyumbani huwa unafanya nini? Vanitha: Huwa napenda kupikapika. Wewe ni mke wa mtu halafu ni sanii, je unapokuwa nyumbani unapenda kumpikia chakula gani mumeo?
Vanitha: Nikiwa nyumbani napenda kumpikia baby wangu chakula kizuri ambacho ni kipya. Ijumaa: Je, pale unapokuwa faragha na mumeo unapenda kumtega kwa vivazi gani?Vanitha: Ukweli huwa simtegi kwa mavazi, napenda kumtega kwa kukaa mtupu kwani wakati huo huwa ni wake, kwa nini nimfichie mali zake?
Ijumaa: Ni upi ugonjwa wako uwapo faragha na huyo mumeo?
Vanitha: Napenda sana kumkumbatia na yeye anikumbatie. Kale kajoto kanakotokea huku tukinong’onezana maneno matamu mimi nabaki kusinziasinzia.
Ijumaa: Watu wanasema wanaume hawatabiriki kwa kuchepuka, hivi siku ukimfumania mumeo utafanya nini?Vanitha: Naomba Mungu isitokee kwani nahisi nitafanya tukio baya na kumuacha siwezi, dah! Nahisi kutetemeka ukiniambia hivyo.
Vanitha Omary akipozi.
Ijumaa: Mastaa wana skendo ya kuchukua waume za watu, wewe unamlindaje mumeo asinaswe na wezi hao? Vanitha: Siwezi kusema nitamlinda kwani sijui mtu anakuwa na nia gani na atakuwa amejipanga vipi ila nabaki kumuomba Mungu amuepushe mume wangu na vishawishi.
Ijumaa: Kuna wanawake ambao eti wanaona kuwapa waume zao mapenzi kinyume na maumbile ndiyo kuwashika, wewe kwako likoje hili? Vanitha: Mungu aniepushie mbali kwani ni jambo baya sana, sijawahi na sitowahi, nawaomba wanaofanya hivyo kuacha kwani Mungu hapendi.
Ijumaa: Ni kitu gani kimewahi kukufurahisha katika maisha yako?
Vanitha: Nilifurahi sana siku niliyofunga ndoa na mume wangu kwani tulipitia mikikimikiki mingi. Tumekaa kwenye uchumba kwa muda mrefu.
Ijumaa: Siku uliyohuzunika sana unaweza kuikumbuka?
Vanitha: Ni siku bibi yangu alipofariki, nakumbuka  nilikuwa katika wakati mgumu kwani yeye ndiye alikuwa mlezi wangu na nilikuwa na ujauzito.
Ijumaa: Mbali na sanaa, ni kazi gani unaifanya?
Vanitha: Mimi ni mbunifu wa kupamba nyumba, nafanya kazi ya kuwadizainia watu nyumba zao kwa mapambo mpaka muonekano mzima wa nyumba .