Aliye kuwa Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Nyerere hivi karibuni aliibua miguno baada ya kumganda kifuani mama wa msanii Elizabeth Michael, Lucresia Karugila huku akionekana kutotaka kubanduka mwilini mwa mama huyo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Nyerere akimbambia mama wa msanii Elizabeth Michael, Lucresia Karugila.
Tukio hilo lililowafanya watu wabaki wakiwa wamepigwa butwaa, lilijiri ndani ya Hoteli ya Landmark jijini Dar kulikokuwa na uzinduzi wa kitabu cha Marehemu Steven Kanumba kiitwacho The Great Follen Tree.
Awali, waalikwa kwenye sherehe hiyo waliinuka na kwenda kucheza wimbo wa Christian Bella wa Nani Kama Mama lakini katika hali ya kushangaza, msanii huyo alikwenda na kumvaa mama Lulu kwa staili ya kumkumbatia kisha kumganda kwa sekunde kadhaa hali iliyoibua maneno.
“Jamani jamani hebu mtazameni Steve alivyoganda kifuani kwa Mama Lulu, dah! Huyu jamaa ana balaa kweli, hata kama ni kucheza au ni salamu ndo amgande mama wa watu vile?’’ alisikika akihoji mmoja wa wadau.