Friday, January 9, 2015
TAMKO RASMI LA WANAUME WA DAR ES SALAAM KUHUSU PANYA ROAD
Baada ya kimya kidogo Ndugu zangu wote wanaume tunaoishi katika jiji hili la Dar es salaam, tumeshuhudia vibweka vya aina yake toka kwa baadhi ya vijana wanaojiita eti wanaume toka huko kanda ya ziwa kutulaani kwa kukimbia eti kuogopa panya road, niseme ukweli kwa niaba ya wanaume wote tuishio hapa hakuna aliyekimbia zaidi ilikua ni kuwatuliza kina mama watoto na wazee kutokana na woga walioingia na kuhofia kujeruhiwa na hao vijana panya road,
Sisi tulikua mstari wa mbele kuwangoja kwenye maeneo yetu ili pindi wakipita tuwashughulikie kisawasawa na si kukimbia kama baadhi ya vijana wa kanda ya ziwa walivyodai, na siku ile hatukulala hadi tulipohakikisha usalama umetulia na hali imekua shwari kabisa. Nawakaribisha wanaume wenzangu wa dar kutoa ya moyoni kwenu hapa dhidi ya udhalilishwaji huu.
Matusi na lugha chafu si msingi wa hoja hii karibuni
-Udaku Special