Staa Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akipozi.
STAA Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond’, amefunguka kwamba haamini kama kweli amepata nafasi ya kutumbuiza kwenye sherehe za utoaji tuzo za wanamichezo bora zilizoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambazo zimefanyika usiku wa kuamkia leo jijini, Lagos, Nigeria.Akizungumza na Showbiz, Diamond alisema amefurahi kupata nafasi ya pekee ambayo mara nyingi hutolewa kwa wasanii wakubwa Marekani na kuamini kwamba muziki wa Tanzania unathaminika kila kona.
“Nimefurahi maana hii inaonyesha jinsi gani muziki wetu umekuwa hadi kufikia Afrika kuwa moja ya kionjo hasa kwenye tamasha kubwa kama hilo, kiukweli sikuwahi kufikiria hapo mwanzo,” alisema Diamond.
Mwaka jana, Diamond aliweka rekodi ya aina yake kwa kupokea tuzo nyingi hapa nchini, ikiwemo tuzo ya Ijumaa Sexiest Bachelor ambayo ilikuwa imedhaminiwa na Kampuni ya Kijumoz Intertraders CO. LTD, ambao pia walitoa ofa ya mshindi huyo mara tu atakaporejea nchini akitokea Nigeria kwenda kwenye maduka yao yaliyopo Kinondoni kwa Manyanya, Kinondoni Mkwajuni na Sinza kufanya shopping ya mavazi kuanzia juu hadi chini.