Friday, January 9, 2015

NI YAYA TOURE TENA MARA YA NNE MFULULIZO MWANASOKA BORA AFRIKA

KIUNGO wa Ivory Coast, Yaya Toure alikuwa ana usiku mzuri Alhamisi ya Januari 8, 2015 baada ya kuvikwa taji la Mwanasoka Bora wa mwaka kwa mara ya nne mfululizo.
Kiungo huyo wa mabingwa wa England, Manchester City ameweka historia hiyo katika sherehe za utoaji tuzo zilizofanyika mjini Lagos, Nigeria.
Mchezaji huyo wa Ivory Coast amewapiku mshambuliaji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang na kipa wa Nigeria, Vincent Enyeama kushinda tuzo hiyo.
Toure alikusanya pointi 175, huku 120 zikienda kwa Aubameyang wakati Enyeama alipata 105.

Katika tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika anayecheza barani, mshambuliaji wa DRC, Firmin Mubele Ndombe aliwapiku Walgeria wawili, Akram Djahnit na El Hedi Belamieri kuibuka kinara. 
Mshambuliaji huyo wa AS Vita alikusanya pointi 136, saba zaidi ya Djahnit, wakati Belamieri alikuwa wa tatu kwa kura zake 126.
Mwanasoka Bora wa Kike Afrika ni kiungo wa Nigeria, Asisat Oshoala, ambaye pia alishinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa mwaka. Super Falcons pia iliteuliwa kuwa timu bora ya taifa ya wanawake.
Algeria imekuwa timu bora ya taifa y Mwaka, wakati, ES Setif imeshinda tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka na koca wao Kheireddine Madoui. Kiungo wa Algeria, Yacine Brahimi ameshinda tuzo ya Mchezaji anayechipukizia vizuri.

WASHINDI WA TUZO ZA CAF 2015

Mwanasoka Bora Afrikan; Yaya Toure (Ivory Coast na Manchester City)
Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika; Firmin Mubele Ndombe (DRC na AS Vita)
Mwanasoka Bora wa Kike;  Asisat Oshoala (Nigeria na River Angels)
Mchezaji Bora Chipukizi; Asisat Oshoala (Nigeria na River Angels)
Anayechipukia Vizuri. Yacine Brahimi (Algeria na Porto)
Kocha Bora wa Mwaka; Kheireddine Madoui (ES Setif)
Timu Bora ya Taifa ya mwaka; Algeria
Timu Bora ya taifa ya Wanawake; Nigeria
Klabu Bora ya Mwaka; ES Setif (Algeria)
Refa Bora wa Mwaka; Papa Bakary Gassama (Gambia)
Kiungozi Bora wa soka wa Mwaka; Moise Katumbi Chapwe – Rais wa TP Mazembe (DRC)
Tuzo ya Gwiji wa Afrika; Oryx Club (Cameroon) – washindi wa michuano Klabu Bingwa Afrika mwake 1964, huku Stade Malien wa Mali ikiwa ya pili.
Tuzo ya Platinum ni Dk Kwame Nkrumah (Rais wa kwanza wa Ghana na Rais wa sasa Nigeria, Goodluck Jonthan.
Kikosi bora cha Mwaka cha CAF ni kipa Vincent Enyeamawakati mabeki ni Jean Kasulula (DRC), Mehdi Benatia (Morocco), Stephane Mbia (Cameroon), Kwadwo Asamoah (Ghana).
Viungo ni Yaya Toure (Ivory Coast), Yacine Brahimi (Algeria), Fakhreddine Ben Youssef (Tunisia), Ahmed Musa (Nigeria) na washambuliaji Asamoah Gyan (Ghana) na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon.
Wachezaji wa akiba ni; Raïs M'Bolhi (Algeria), Firmin Mubele Ndombe (DRC), Ferdjani Sassi (Tunisia), Yao Kouasi Gervais ‘Gervinho (Ivory Coast), Abdelrahman Fetori (Libya), Akram Djahnit (Algeria), Roger Assalé (Ivory Coast).