Vijana wanaounda Kundi la Wasafi Classic linaloongozwa na Diamond Platnumz wakiwasili katika ofisi za Global Publishers Ltd leo.
BAADHI ya vijana wanaounda Kundi la Wasafi Classic Baby 'WCB' linaloongozwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz', leo wametembelea ofisi za Kampuni ya Global Publishers Ltd, Mwenge-Bamaga jijini Dar.
Vijana hao wakiongozwa na mmoja wa mameneja wao, Babu Tale wamepata fursa ya kuongea na wanahabari wa Global na kuelezea mipango yao ya mwaka huu pamoja na mafanikio waliyoyapata kupitia muziki.
Akizungumza na mtandao huu, Babu Tale amesema, "WCB kwa mwaka huu wamejipanga kufanya makubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kufungua kampuni, kuzindua tovuti ya staa Diamond Platnumz na mambo mengine kibao yahusuyo muziki".