Tuesday, January 27, 2015

WEMA SEPETU APIGIWA MAGOTI NA GAZETI LA MTANZANIA NA KUOMBWA MSAMAHA

“Katika gazeti letu la Mtanzania toleo No. 7709 la
Alhamisi Januari 22, mwaka huu, tuliandika
kimakosa stori yenye kichwa cha habari ‘Wema
Sepetu ampeleka Diamond Polisi’. Baada ya
kufanya uchunguzi tumejiridhisha habari ile
haikuwa na ukweli, kwani chanzo kilichotupatia
kilitupotosha, hivyo kuleta usumbufu kwa msanii
Wema pamoja na jamii. Kutokana na hali hiyo,
tunapenda kumwomba radhi Wema na familia
yake. Siku zote sisi MTANZANIA tumekuwa
makini katika kusimamia misingi ya habari za
weledi na haki kwa jamii”. Mwisho wa kunukuu
Kitendo cha kumuomba msahani mwanadada
Wema ni kitendo cha kiungwana pongezi kwenu
Mtanzania natumai Wema kwa uungwana wake
atawaelewa.