Sunday, January 4, 2015

WOLPER ANAPENDA SANA KUCHEZEA HII KITU HAPA!


Hakuna anaeweza kupinga kuwa mrembo na moja kati ya waigizaji pendwa wa kike hapa bongo, Jackline Masawe “Wolper”ni miongoni mwamastaa wa kike wachache ambao wanapenda kubadilisha mitindo ya nywele zao mara kwa mara. 
Kwa wanaomfuatilia mitandaoni watakubali kuwa haiwezi ikapita wiki bila mwanadada huyu kuonekana na “style” mpya ya nywele.
Hatimaye leo akiwa katika mtindo mpya (picha hapo juu) wa nywele, wolper alifunguka na kusema kuwa yeye anapenda kuchezea kichwa chake na kuwaonya watu wasimuige kwani yeye yupo tayari kwachangamoto atakazo zipata uzeeni.
“Me napendaga tuu kukichezea hiki kichwa changu jamani nando furaha yangu ..sasa we jipenicshe na kichwa changu wakati me sijali ila nasikitika tuu uzeeni kma Mungu akiniweka weka hayo maumivu yake yakichwa na ubongo". Wolper alimaliza.