Monday, February 9, 2015

ESTER: NINA ‘PROJECT’ NA DUDE!

MSANII wa filamu anayechipukia Bongo, Ester Kiama, amefunguka kuwa ukaribu wake na mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’ ni kwa sababu ana ‘project’ ya kazi anafanya na staa huyo.
Msanii wa filamu anayechipukia Bongo, Ester Kiama akipozi.
Akizungumza na mwandishi wetu, Ester alisema ameshangaa kusikia watu wakieneza habari kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Dude wakati amemfuata msanii huyo mkubwa ili amsaidie akue.
 “Jamani hakuna mapenzi zaidi ya ka-project ka kazi ambako ananisaidia mimi ili niweze kukua kisanaa, kikubwa nahitaji sapoti ya kisanaa,” alisema Ester.