Friday, February 13, 2015

Hali ya hewa ilipochafuka wakati Rais Zuma akihutubia Bunge South Africa…

Members of Julius Malema's Economic Freedom Fighters (EFF) clash with security officials after being ordered out of the chamber during President Jacob Zuma's State of the Nation address in parliament in Cape Town
Wabunge wenzake na Julius Malema wenye nguo nyekundu wakitolewa nje ya Bunge Afrika Kusini jana jioni February 12
Hali ya hewani kuchafuka Bungeni hii Duniani kote iko, ukiyaona leo Bongo sio mageni, kuna wakati utayaona hayo hata kwenye Mijengo ya Mabunge ya wenzetu yaani.
Leo kubwa iliyokaa kwenye kurasa za mbele Magazetini, mitandaoni, ishu ya Wabunge wa upinzani Afrika Kusini kumkatisha Rais Zuma wakati akihutubia Bungeni jana jioni FEBRUARY 12 na kuanzisha mzozo mkubwa wakimtaka Rais huyo aeleze kuhusu tuhuma za Rushwa na Ufisadi zinazomkabili.
Tunamtaka Rais atujibu majibu mepesi; lini atarudisha pesa zetu“– alihoji Mbunge wa Upinzani, Julius Malema.
BN-GY077_ZUMAjp_M_20150212135208
Julius Malema akiongea na waandishi wa habari baada ya kutolewa Bungeni.
Spika wa Bunge Baleka Mbete alimtaka Malema kutoka nje ambapo baada ya kuonekana akibisha kundi la askari walivamia na kumtoa kwa nguvu ndani ya Jengo hilo pamoja na baadhi ya Wabunge, ambapo baadaye Rais Zuma aliendelea na hotuba yake.
BN-GY073_ZUMAjp_M_20150212134323
Askari wa Bunge wakiwa nje ya Jengo la Bunge kuangalia usalama baada ya Wabunge hao kutolewa nje.
Mwezi Novemba 2014 Mbunge Mashabela aliwahi kutamka ndani ya Bunge hilo kuwa Rais Zuma ni mwizi hali ambayo ilichafua pia hali ya hewa kwenye Bunge hilo kwa kiasi kikubwa.
Hii ni video ya tukio la mwaka 2014.