Hebu pata picha, mtu analalamika kwamba anaumwa, akapewa kitanda Hospitali kwa ajili ya kupata matibabu, madaktari wanamwambia vipimo vinaonyesha kapona kabisa lakini yeye anasema bado anaumwa.
Huyu ni mtu mzima mwenye umri wa miaka 41 kutoka China, jina lake ni Chen alipata ajali mwaka 2011 akalazwa Hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya miguu, baadaye madaktari waliona vipimo vikionesha hali yake iko poa, amepona kabisa.
Kitu cha ajabu ni kwamba yeye alidai bado anaumwa sana miguu, hawezi hata kutembea lakini madaktari walimpima na hawakuona tatizo lolote kwenye miguu yake.
Aligoma kutoka Hospitali na kali zaidi ni kwamba alijifunga mnyororo yeye mwenyewe kwenye kitanda alicholala Hospitali hapo kwa miaka mitatu, akilalamika anaumwa, hakuwahi hata kuoga kwa kipindi hicho chote.
Uongozi wa Hospitali wakaona isiwe tabu, wakaenda kumshtaki kituo cha Polisi, askari wakafika Hospitali wakakata mnyororo aliojifunga kwenye kitanda na kumtoa Hospitali hapo kwa nguvu huku wamembeba juu juu.
Mwenyewe amelalamika kwamba bado anaumwa, mpango wake kwa sasa ni kufungua mashtaka ili mahakama itoe kibali afanyiwe vipimo upya aendelee na matibabu.
Hapa kuna pichaz zote askari wakimalizana na jukumu la kumtoa kwa nguvu mzee huyo hospitali.