Friday, February 13, 2015

MWIZI AKAMATWA CHUO KIKUU MZUMBE ANUSURIKA KIFO NA WANAFUNZI WENYE HASIRA KALI -MOROGORO







polisi wakifanya jitihada za kumshusha mwizi kutoka gorofani alipokuwa akiiba


mwizi kishushwa chini ya hostel ya mkwawa akiwa chini ya ulinzi mkali wa askali polisi

mwizi akiingizwa kwenye gari la chuo tayari kupelekwa kituoni

wanafunzi wakiwa na jazba kubwa ya kutaka kumuua mwizi huyo anayesoma mwaka wa pili chuoni hapo




chumba kilichopo sammit hostel ya mkwawa ambacho mwizi huyo alipokuwa amefungiwa kwa nje mara baada ya kuingia ndani kwa kutumia funguo malaya ikisadikiwa kuwa anataka kuiba laptop.

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa wanafunzi wa chuo kikuu mzumbe jioni hii wanusurika kumuua mwanafunzi mwenzao ambae anasoma mwaka wa pili chuoni hapo kwa kufanya jaribio la kuiba katika chumba namba 403 kilichopo gorofani sammit katika hosteli ya Mkwawa kwa kufungua mlango kwa funguo malaya ambapo inasemekana kumbe ndani kulikuwa na mtu na ndipo alipoingia ndani na kuwekwa chini ya ulinzi na kufungiwa kwa nje, uongozi wa chuo kwa kushirikiana na mama dean wa chuoni hapo na uongozi wa serikali ya wanafunzi ndipo ulipoamua kuita polisi na kufanikiwa kumtoa kwa utata kwa kuwa wanafunzi walikuwa na hasira kali ya kutaka kumuua.

Chuo kikuu mzumbe ni chuo kimojawapo Tanzania ambacho kinakabiliwa na tatizo la wizi wa Laptop ambapo inasemekana kwa kipindi hiki cha mitihani kwa week huibiwa wastani wa laptop tano ambapo inadaiwa hata leo hii siku ya tukio imeibiwa laptop moja huku mwenyewe mali akiwa katika chumba cha mtihani.