Friday, February 13, 2015

JE, KWA HILI JB NA KAMPUNI YAKE YA JERUSALEM WAMETELEZA AU ?

Je, kwa Hili JB na Kampuni Yake ya Jerusalem Wameteleza Au ?

 Haya ni maoni ya mwanasheria kijana,  kuhusu makosa ya uandishi wa lugha ya kinegereza kwenye kasha la filamu ya Mzee wa Swaga, iliyotengenezwa na kampuni ya Jerusalem, inayomilikiwa na msanii nguli wa filamu, Jacob Stephen JB.
Alberto aliandika haya mara baada ya kupandika picha hiyo ya kwenye kasha na kuandika haya;
“Bado ni marafiki zangu tu. Ninachotaka ni sanaa yenu ipendwe na watanzania waithamini. Soko la ndani ni kubwa sana. Ila endapo tu mtazingatia ubora. Najua mtaji wa kuwekeza kwenye filamu ni kazi kuupata. Basi hayo makubwa tuyaache. Tubaki na haya madogo ambayo yako ndani ya uwezo wenu. Hakuna from produced of shikamoo mzee. Na hakuna enterianments. Kiswahili ni sawa pia kutumia. Kwani ingeandikwa 'Imeandaliwa na' kuna shida? Na hakuna auto correct ya entertainment? UTASIKIA utetezi wa kitoto; sio lugha yetu!! Au ni bahati mbaya!”-Alberto alimaliza
Una maoni gani juu ya hili.