Wednesday, February 4, 2015

KAJALA:ACHENI AKILI ZA KIJINGA MAVAZI YANGU HAYA HARIBU TABIA YA MTOTO WANGU, KAMA ATAARIBIKA KWA KUNIONA NIMEVAA TUMBO WAZI BASI NI MBUMBUMBU

Udaku Special-Kajala ameshindwa Kujizuia na kuamua kuwashukia wale wote wanaosema anamwaribu mtoto wake kwa Mavazi anayovaa...Soma alichoandika hapa chini:

"Naomba niwaulize binadamu alie kwambia mimi nikivaa hivi nitamuhalibu mtoto nani ? acheni akili za kijinga kwasababu wengi wetu tunajua kabisa mtoto hawi na tabia mbaya kwasababu anamuona mama yake kavaa dira au tumbo wazi sisi zamani wazazi wetu walikuwa wanavaa hivi lakini mbona tuliwasumbua mnaboa na kukera pia kama mtoto wangu atahalibika kisa kaniona mimi nimevaa tumbo wazi utakuwa ni umbumbu wake na ujinga wake lakini sidhani kama mavazi yanamualibu mtoto naisi nimalezi peke yake kama nakuboa usipite hapa tafadhali".

Kajala aliandika na kutupia picha hiyo juu mtandaoni.

Je Wewe Unamaoni Gani?