Mvulana mmoja amefanyiwa kile madaktari wanasema ni upasuaji wa kwanza wa kupunguza uume wake.
Kijana huyo wa miaka 17 alikuwa akilalamika kwamba hangeweza kushiriki katika tendo la ngono ama hata kushiriki katika michezo swala lililomshinikiza kuomba kupunguzwa uume wake.
Kabla ya kufanyiwa upasuaji huo uume huo ulikuwa na urefu wa nchi 7 na ukubwa wa nchi 10.
Daktari wa upasuaji Surgeon Rafael kutoka chuo kikuu cha Florida kusini ambaye alifanya upasuaji huo aliliambia gazeti la mail online kwamba ''kuna wakati ambapo kila daktari wa upasuaji hupata ombi la maajabu linalokuwacha kinywa wazi.
''Swali hilo ni Je, unaweza kuufanya uume wangu kuwa mdogo''?.
Kwa wale waliohitaji kufanyiwa upasuaji huo, uume wao haui mkubwa wakati unapodinda bali huwa mgumu.
Daktari huyo alisema kwamba wengu hufanyiwa upasuaji wa kukiongeza kiungo hicho na wala si kukipunguza.
Kijana huyo alifanyiwa matibabu hayo na kumaliza matatizo yake.