Thursday, February 12, 2015

PENNY ATAJA MAHARI KWA MWANAUME ALIE TAYARI....


Jina la Penny limo katika orodha ya mastaa waliowahi kuwa na uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. Jina lake kamili ni Penniel Mwingilwa. Huyu ni Mtangazaji wa Radio Efm ya jijini Dar. 

Mtangazaji wa Radio Efm ya jijini Dar Penniel Mwingilwa.
Wiki hii yuko hapa kujibu maswali ambayo waandishi wetu Imelda Mtema na Hamida Hassan walimuweka mtu kati.Ijumaa: Mambo Penny, naona sasa hivi una gari nyingine, ile Toyota Brevis ambayo mpenz wako wa zamani Diamond alikununulia iko wapi?
Penny: (Kicheko)...kwa kweli namshukuru kwa kuninunulia ile gari ila sasa hivi siko nayo, nimeamua kubadilisha, si unajua mtu lazima uende na wakati?
Ijumaa: Mara ya mwisho kupanda daladala ilikuwa lini?
Penny: Nakumbuka ilikuwa mwaka 2008. Nilipoanza tu kazi ya utangazaji, nilipopanda daladala watu walikuwa wananishangaa sana nikaona hiyo siyo poa, nikawa napanda teksi.
Ijumaa: Ulikuwa na Diamond mkaachana, hebu tuambie kwenye maisha yako ungependa umpate mwanaume wa aina gani?Penny: Kwanza awe mchamungu, pili anithamini lakini pia awe mtu muelewa. Yaani ajue ni wakati gani wa kufanya maamuzi sahihi na awe tayari kunisikiliza.
Ijumaa: Nini ambacho kinakukwaza sana na hukipendi kabisa?
Penny: Ni watu kuniongelea tena kwa mambo ambayo hawayajui kuhusu mimi. Nakerwa sana na wanaofanya hivyo.Ijumaa: Ukiwa katika ‘stress’ au mtu kakukwza na kukukosesha amani, kipi ambacho huwa unakifanya kurudisha amani yako?
Penny: Nikiwa katika hali hiyo breki ya kwanza ni kanisani. Pale kwenye Kanisa la St. Joseph pembeni kuna kakanisa kadogo.Kwa hiyo nakwenda pale, nasoma Biblia na kusali kwa muda wa saa sita hivi kisha nikiondoka hapo nakuwa sawa.
Ijumaa: Muda wa kuolewa ukifika na mwanaume akaja kwenu na ukatakiwa utamke mwenyewe mahari yako, ungetaka mahari ya shilingi ngapi?Penny: Sina makuu, nitamtaka mwanaume huyo ampe baba yangu juzuu na msahafu halafu mama yangu apewe Biblia. Kama kutakuwa na pesa kidogo tutaipeleka kwa watoto yatima.
Ijumaa: Mastaa wengi wa kike wanadaiwa kutojua kupika, wewe hili likoje kwako?
Penny: Kitu ambacho nitamshukuru mama yangu siku zote ni kunifundisha kupika. Najua kupika vitu vingi sana tena vinakuwa vitamu mno, kasoro ugali ndiyo unanishinda ila najitahidi kujifunza.
Ijumaa: Umeanza kujitegemea ukiwa na umri mdogo, vipi unajilindaje na vishawishi vya wanaume?
Penny: Wakati naanza kupanga tulikaa kama familia, tukajadili ikaonekana naweza kukaa peke yangu japo bado nipo chini ya wazazi wangu. Kuhusu vishawishi havinisumbui kwani najitambua.
Ijumaa: Kilichowasukuma mkaamua kupatana na Wema Sepetu ni kipi?
Penny: Sisi ni watu wazima, tuliona haileti picha nzuri kuwa maadui. Sasa hivi tuko na amani na hatutaruhusu watu watugombanishe tena.
Ijumaa: Ni kwa nini unapenda kuvaa nguo fupi?
Penny: Vimini siwezi kuacha ndugu yangu kwa sababu nina mguu mzuri wa kuvaa hivyo, au wewe unanionaje?