Monday, February 2, 2015

MADAHA AVUTIWA NA FREEMASON

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ametoa kali ya aina yake baada ya kusema anavutiwa na taasisi huru ya imani ya Freemason kutokana na umakini mkubwa walionao kwenye kazi zao. Akipiga stori na paparazi wetu, Baby alisema watu wengi wamekuwa wakizungumza kwa mitazamo tofauti kuhusiana na Freemason lakini kiuhalisia, watu wa imani hiyo ni makini wanaojitambua na kujiheshimu.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha akipozi.
“Hawa jamaa kiukweli siyo wa kuchezewa kabisa, lakini ukweli tu ni kwamba nawazimikia mno na ndiyo sababu mara nyingi hata ukiangalia kazi zangu za muziki utakutana na nembo zao kivyovyote vile, sema siwezi kujiunga nao,” alisema Baby Madaha.