Tuesday, February 3, 2015

Majibu ya Aunt Ezekiel kuhusu kuwa na ujauzito wa dancer wa Diamond, ndoa yake je?

.
.
Mengi yamezungumzwa kwenye mitandao  na kuchukua headline kuhusu Ujauzito wa Muigizaji wa filamu, Aunt Ezekiel, sasa leo Feb 2 kupitia Amplifaya ya Clouds FM Aunt Ezekiel amefunguka na kujibu baadhi ya maswali haya.
Millardayo:..’Vipi kuhusu Ndoa yako kwasababu uliolewa na Mtanzania aishie Dubai?
Aunt Ezekiel:..”Ndoa yangu bado ipo na itaendelea kuwepo na still bado mume wangu bado yupo..”
Millardayo :..Kulikuwa na taarifa kuwa amefungwa gerezani..?”
Aunt Ezekiel: “Sipendi sana kukiongea hicho kwasababu kama nilivyosema mwanzo kwamba maisha yangu binafsi uwa ni  maisha binafsi ambapo yakija ya usanii yanakuwa ya usanii, kwa hiyo hayo ni maisha yangu binafsi ila kwa kifupi sijaachika na ndoa ipo na itaendelea kuwepo…”
Millardayo:..”Na kuna taarifa kwamba una ujauzito wa Moze ambaye ni dancer wa Diamond Platnumz is it true…?”
Aunt Ezekiel:...”Mimi mwenyewe nasoma kwenye magazeti , nasikia kwenye radio kama wewe unavyosema hivyo yaani lakini mimi binafsi ndio najua hii mimba ni ya nani..”
Unaweza uka bonyeza play hapa chini kuisikiliza interview yenyewe.