MSHEHERESHAJI wa onyesho la Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ kumpongeza mwimbaji kiongozi Luiza Mbutu kutimiza miaka 16 ya kuifanyia kazi mfululizo bila kuhama, Sakina Lyoka, Jumamosi iliyopita alimkera mgeni rasmi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenela Mkangara baada ya kukosea kutamka vizuri cheo chake.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenela Mkangara (kushoto) akiwa na Luiza Mbutu.
Mtangazaji huyo wa televisheni, wakati akimkaribisha, alimtambulisha kama Waziri wa Utamaduni, kitu ambacho kilimkera kiasi cha kumnyang’anya kipaza sauti ili kumsahihisha.
“Jamani mimi naitwa Fenela Mkangara, ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na siyo Waziri wa Utamaduni kama alivyonitambulisha huyu Mc,” alisema Waziri huyo ambaye baadaye alimpongeza Luiza kwa kudumu kwa muda wote bila kuhama na kuonyesha nidhamu kazini.