Wednesday, February 4, 2015

Mwanasheria Mkuu Asema Serikali Haina Dini Mahakama ya Kadhi itahudumiwa na Waislam wenyewe

Udaku Special:Akizungumza kupitia taarifa ya habari Itv Mwanasheria Mkuu ametangaza Rasmi kuwa Mahakama ya Kadhi itahudumiwa na Waislamu Wenyewe.



Amesema kuwa Serikali haina Dini na Kamwe haitajihusisha na maswala ya imani za Kidini.

Mwanasheria pia amesema kuwa Mahakama hiyo ilishakuwepo na ilikuwa ikihudumiwa na Waislamu wenyewe.

Hii ni Habari njema sana kwa wale wote ambao walikuwa wanajisikia vibaya kugharamia Dini isiyokuwa yao.

Naipongeza sana Serikali kwa kuamua hivyo.

Mungu ibariki
Tanzania.