Sunday, February 15, 2015

Mwendelezo wa taarifa kuhusu waliofariki kwenye ajali ya TransAsia

0023ae9885da1640037606
Mpaka siku ya jana February 12 idadi ya miili ya marehemu waliofariki na kupatikana kwenye ajali ya ndege ya TransAsia Airlines GE235 ambayo ilianguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege Taipei ilikuwa ni maiti za watu 42, pamoja na majeruhi 15 huku kukiwa na taarifa kwamba mwili wa mtu mmoja bado haujapatikana.

Leo vikosi vya uokoaji vimefanikiwa kuupata mwili wa mtu mmoja ambao haukuwa umepatikana mpaka jana.
Ndege hiyo ilipata hitilafu kwenye engine moja na kufanya ndege hiyo kupoteza mwelekeo, ikagonga ukingo wa daraja na kuanguka mtoni.
Siku ya juzi ndugu wa marehemu walikaa kikao na uongozi wa Kampuni hiyo ya ndege na kukataa kulipwa fidia ya pesa ambayo ni sawa na jumla ya dola milioni 14.9 za Taiwan (zaidi ya Ths. Milioni 850/-) ambayo wangepatiwa ndugu hao kwa kila mtu mmoja aliyefariki kwenye ajali hiyo.