MTANGAZAJI na muigizaji wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ amezua tafrani la aina yake baada ya kutinga kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Mwananyamala jijini Dar akiwa nusu utupu.
Tukio hilo lilitokea juzikati ambapo Lulu alipoingia alipita katikati na kwenda katika kaunta ya baa hiyo huku akijitingisha makusudi na kusababisha wanaume waliokuwa wamekaa kwenye baa hiyo wapige kelele wakimtaka aondoke.
“Hii sasa ni sifa haiwezekani atuvalie kigauni kifupi namna hii, akibakwa atasemaje? Hatukubali, bora ingekuwa usiku, tumwambie mwenye baa kama anataka amtoe huyu au sisi tuondoke, hata kama tuko baa lakini tunajieheshimu,” alisikika mmoja wa wanaume hao.
“Huu ujinga bwana sisi tunajiheshimu, hawezi kuvaa hivi tena inaonesha hana hata kufuri, bora niondoke eneo hili,” alisikika mwanaumwe mwingine na kuondoka zake.Hata hivyo, meneja wa baa hiyo aliwasihi watu kubaki na kumvumilia lakini wengi wao waliamua kuondoka kwa hasira.
Waandishi wetu walipomuuliza sababu ya kufika pale na kiguo hicho alisema kuwa alifika kwa mambo yake muhimu na kukutana na rafiki zake Isabela Mpanda ‘Bela’ na Baby Madaha hivyo kama wateja wengine wamemsusuia, watajijua.