Mrembo na mwigizaji wa filamu, Shamsa Ford amewabwatukia baadhi ya watu ambao wanapenda kumsema kuwa yeye ni mshamba kwa kushindwa kutoka misele nyakati za usiku.
Shamsa alisema anawashangaa watu hao kumsema na kumjadili kwa watu wengine kuwa yeye ni mshamba kitu ambacho hakipendi kwani kila mtu ana aina yake ya maisha aliyoyachagua kuishi.
“Mimi sijawahi kumsumbua mtu hela ya kula hata siku moja kisa tu eti sijichanganyi na wanawake wa mjini, mimi familia yangu ndiyo namba moja, ndivyo nilivyoamua kuishi mtu akiniiita mshamba atakuwa anajisumbua tu,” alisema Shamsa.