Monday, February 9, 2015

WASTARA AWACHARUKIA WANAOMTUSI MUME WAKE

MSANII mkongwe katika gemu la filamu
Bongo, Wastara Juma ameapa kumshtaki mtu
atakayekamata kutokana na baadhi ya
mashabiki kuwa na tabia ya kumtukana matusi
ya nguoni mtandaoni huku wakimhusisha na
marehemu mumewe , Sajuki .
Msanii mkongwe katika gemu la filamu Bongo,
Wastara Juma.
Akizungumza na gazeti hili , Wastara alisema
anajisikia vibaya baadhi ya mashabiki
wanavyomtukana kwenye mitandao ya kijamii
jambo ambalo siyo zuri kwani wanaingilia
maisha yake binafsi na kibaya zaidi
wanamhusisha Sajuki .
“ Ukweli sipendi kabisa na nitamshtaki mtu
maana wananitengenezea chuki kwani wakati
mwingine wananitukana , wanamtukana sana
Bondi huku wakidai kwamba nilikuwa naomba
Sajuki afe ndiyo nifanye mabaya sasa sijui
nimefanya kitu gani kibaya, kuwa na Bondi
nimekuwa naye baada ya mume wangu
kufariki maana mimi ni binadamu na kama
angekuwepo nisingekuwa na mwanaume
mwingine zaidi yake, ” alisema Wastara .