Sunday, March 29, 2015

AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA KWA KOSA LA KUMUOA DADA YAKE ALBINO HUKO KAHAMA


Mahakama ya wilaya ya kahama mkoani Shinyanga Jana imemuhukumu kwenda jela miaka 20 Ally Sanyiwa (24) kwa kosa la kumuoa dada yake Mektilda Sanyiwa(20) mkazi wa Chela.

Imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi Koplo Evodia mbele ya hakimu mfawidhi George Mariki kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mwezi machi mwaka huu.

Aidha koplo Evodia ameiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo aliweza kumtorosha dada yake na kisha kumpeleka katika kijiji cha Mazimba na kuishi naye.

Wazazi wa Mektida ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) wamesema kuwa mara baada ya binti yao kutoweka nyumbani walipata hofu na kuanza kumtafuta mpaka alipopatikana akiwa anaishi nyumba moja na kijana wao.

Mahakama hiyo imetoa hukumu kwa mtuhumiwa huyo mara baada ya kukiri kutenda kosa hilo ambalo ni kinyume na maadili ya kitanzania.