Sunday, March 29, 2015

Tanzia!! - ABDUL BONGE WA TIP TOP CONNECTION AFARIKI DUNIA,MCHEKESHAJI MAARUFU DIFENDA NAYE AFARIKI

Abdul Bonge enzi za uhai wake.
ALIYEWAHI kuwa Meneja wa wasanii na mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Chanzo cha kifo cha Abdul Bonge bado hakijafahamika ila msiba upo Manzese Tip Top.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN
Wakati huo huo kuna taarifa kuwa mchekeshaji maarufu kwa jina la Difenda naye amefariki dunia,Tunafuatilia kwa ukaribu zaidi kuhusu taarifa hizo tutawaletea taarifa kamili hivi punde