WATU kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha baada ya basi la Nganga la kutoka Dar kwenda Mbeya kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso maeneo ya Mlimani kilometa kadhaa kutoka Ruaha-Mbuyuni, katika barabara ya Iringa-Morogoro ambapo magari yote mawili yameteketea kwa moto.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kwamba mmoja wa watu waliofariki ni dereva wa Fuso.